Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:19

Biden analaani ukatili wa Putin ndani ya nchi ya Ukraine


Hali katika eneo la Bucha mji mkuu wa Kyiv nchini Ukraine
Hali katika eneo la Bucha mji mkuu wa Kyiv nchini Ukraine

Rais wa Marekani Joe Biden alitamka Jumatatu kuwepo kwa kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya Rais wa Russia Vladmir Putin na kulaani ukatili unaodaiwa kufanywa na wanajeshi wa Russia ambao umegunduliwa siku za karibuni huko Bucha kitongoji cha mji mkuu wa Kyiv nchini Ukraine.

Unaweza kukumbuka kwamba nilikosolewa kwa kumwita Putin mhalifu wa kivita, Biden aliwaambia waandishi wa habari huko White House. Ukweli wa mambo mmeona kilichotokea Bucha.

Hii inathibitisha yeye ni mhalifu wa vita. Lakini tunapaswa kukusanya taarifa. Mtu huyu ni katili na kinachotokea Bucha ni cha kuudhi na kila mtu amekiona, Biden alisema.

Miili ya raia 410 imeondolewa katika miji ya eneo la Kyiv ambayo ilichukuliwa tena hivi karibuni kutoka kwa vikosi vya Russia, mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine Iryna Venediktova alisema.

Wakati huo huo Rais wa tume ya ulaya, Ursula von der Leyen, ali tweet Jumatatu kwamba Umoja wa Ulaya utatuma wachunguzi nchini Ukraine kumsaidia kunakili uhalifu wa kivita.

XS
SM
MD
LG