Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:09

Mwanamfalme Hamza wa Jordan ametangaza kuachia cheo chake


Mwanamfalme Hamza bin al-Hussein wa Jordan. Agosti 21, 2004.
Mwanamfalme Hamza bin al-Hussein wa Jordan. Agosti 21, 2004.

Mwanamfalme Hamza bin al-Hussein, mrithi wa zamani wa kiti cha ufalme cha Jordan ambaye alikua katika kifungo cha nyumbani hapo mwaka 2021 alitangaza Jumapili kwamba anaachia cheo chake cha ufalme huku akipinga sera za sasa za Jordan.

Hamza alishtakiwa April mwaka jana kwa kujaribu kuvuruga utawala wa kifalme katika njama iliyochochewa na wageni, lakini aliepuka adhabu baada ya kuahidi kumtii mfalme Abdullah ambaye ni kaka yake wa kambo.

Katika barua hiyo iliyochapishwa kwenye akaunti ya Twitter, Hamza alisema kile alichokishuhudia katika miaka ya karibuni kilimfanya kuwa mgumu kuidhinisha sera zinazofuatwa na taasisi za Jordan. Nimefikia hatima kwamba Imani yangu binafsi na kanuni alizoziweka baba yangu, marehemu Mfalme Hussein haziendani na njia, maagizo, na mbinu za kisasa za taasisi zetu, aliandika.

Hamza mwenye miaka 42 alitajwa mwana mfalme wakati Mfalme Hussein alipofariki mwaka 1999 na Abdullah akawa mfalme lakini alipoteza cheo hicho miaka mitano baadae, wakati Abdullah alipomuweka mtoto wake mwenyewe wa kiume kama mrithi.

XS
SM
MD
LG