Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 14:41

Msalaba Mwekundu inaonya kuwepo tatizo la hali ya afya Ukraine


Baadhi ya magari ya Shirika la Msalaba Mwekundu katika maeneo yenye mgogoro wa vita
Baadhi ya magari ya Shirika la Msalaba Mwekundu katika maeneo yenye mgogoro wa vita

Shirikisho la kimataifa la Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu linaonya kuhusu tatizo la afya linaloendelea nchini Ukraine ambalo huenda likadumu kwa muda mrefu zaidi kuliko mzozo wenyewe.

Francesco Rocca, rais wa shirikisho la Msalaba Mwekundu aliitembelea Ukraine na Romania kuona hali katika eneo hilo tangu jeshi la Russia lilipoivamia Ukraine wiki tano zilizopita.

Anasema hakuna mtu nchini Ukraine ambaye ameachwa bila kuathiriwa na mzozo unaoendelea. Anakadiria watu milioni 18, au theluthi moja ya watu watahitaji msaada wa kibinadamu. Zaidi ya hayo, anasema takribani watu milioni 6.5 wamekoseshwa makazi ndani ya nchi na zaidi ya milioni nne wakimbizi katika nchi jirani watahitaji misaada ya kimataifa.

Ameelezea wasi-wasi wake juu ya kile anachokiona kama tatizo la afya linaloibuka. Anasema mamilioni ya watu hawana tena fursa ya huduma ya afya na matibabu kwa sababu ya mashambulizi kwenye mahospitali magari ya kubeba wagonjwa na wafanyakazi wa afya.

Shirika la afya duniani (WHO) linasema zaidi ya vituo 70 vya afya vimeshambuliwa na baadhi vimeharibiwa. Takriban watu 71 wameuawa, na 37 walijeruhiwa.

Anasema wafanyakazi wa kujitilea wa Msalaba mwekundu, wao wenyewe wameathiriwa na mgogoro huo. Anasema wengi wamepoteza nyumba zao, jamii na wapendwa wao. Licha ya huzuni yao ya kibinafsi, anasema wanaendelea kufanya kadri wawezavyo kuwasaidia na kuwafariji waathiriwa wa vita hivi vibaya. Tangu mwanzo wa vita hapo Februari 24 anasema wafanyakazi wa kujitolea wa Msalaba Mwekundu wamewasaidia zaidi ya watu 400,000 nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG