Serikali ya Ethiopia siku ya Alhamis ilitangaza haraka sitisho la mapigano la upande mmoja katika mzozo wake na waasi wa Tigray ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia katika jimbo la kaskazini ingawaje haiko bayana jinsi sitisho hilo litakavyoimarishwa.
Ilisema ina matumaini sitisho hili litaboresha kwa kiwango kikubwa hali ya kibinadamu katika eneo hilo na kufungua njia ya kupatikana kwa suluhisho kwa mzozo huo wa kaskazini mwa Ethiopia bila ya umwagaji damu zaidi, serikali ilisema katika taarifa yake.
Tangu vita vilipozuka kaskazini mwa Ethiopia hapo Novemba 2020 maelfu wamekufa na wengi zaidi wamelazimika kukimbia makazi yao huku mzozo huo ukipanuka kutoka Tigray hadi mikoa jirani ya Amhara na Afar.
Serikali ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ina nia ya dhati kutumia juhudi kubwa kufanikisha uingiaji wa misaada ya dharura ndani ya mkoa wa Tigray, ilisema taarifa. Ili kuboresha mafanikio ya usitishaji vita wa kibinadamu. Pia inatoa wito kwa waasi huko Tigray kuacha vitendo vyote vya uchokozi na kuondoka katika maeneo ambayo wanayakalia kimabavu katika mikoa jirani ilisema taarifa.
Hata hivyo serikali ya Ethiopia inatumai kwamba sitisho hili hatimaye litaimarisha kwa kiasi kikubwa hali ya kibinadamu huko na kufungua njia ya kupatikana suluhisho kwa mzozo wa kaskazini mwa Ethiopia bila umwagaji damu zaidi.