Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 19:56

Watu 24 wamejeruhiwa na mmoja kuuawa huko Arkansas Marekani


Ufyatuaji risasi ulifanyika katika jimbo la Arkansas nchini Marekani

Mtu mmoja aliuawa na 24 wengine walijeruhiwa wakati milio ya risasi ilipolipuka wakati wa maonyesho ya magari ambayo ni sehemu ya tukio la kila mwaka la jumuiya katika mji mdogo wa kusini mashariki mwa jimbo la Arkansas nchini Marekani mamlaka ilisema Jumapili.

Polisi hawajasema kilichopelekea shambulizi hilo la risasi lililotokea Jumamosi usiku huko Dumas lakini gavana Asa Hutchinson alisema kwenye twitter kwamba kulikuwa na washukiwa wawili mmoja wao amekamatwa na anashikiliwa kwa mashtaka yasiyohusiana na tukio hilo.

Takribani watoto sita walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa. Wakati uchunguzi ukiendelea, nitaangalia maelezo ili kuona ikiwa kuna hatua zozote ambazo zingeweza kuchukuliwa kuzuia maafa ya aina hii, alisema Hutchinson.

Dumas ni jiji lenye wakaazi 4,000 lililopo kiasi cha kilometa 144, kusini mwa Little Rock. Maonyesho ya magari ni sehemu ya hafla ya jumuiya inayofanyika kila mwaka katika majira ya Spring yanaitwa Hood-Nic ambapo ni kifupi cha “pikniki ya ujirani”.

Taasisi ya Hood-Nic ilisema kwenye tovuti yake kwamba dhamira yake ni kujenga upya, kuungana tena, na kujibu mahitaji ya vijana katika jumuiya zetu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG