Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 18:05

Umoja wa Mataifa waionya Libya kuhusu mapigano mapya


Fathi Bashagha, Waziri Mkuu mpya wa Libya aliyechaguliwa na bunge la nchi hiyo akila kiapo huko Tobruk

Umoja wa Mataifa siku ya Alhamis ulionya dhidi ya “chokochoko” nchini Libya ambazo zinaweza kusababisha mapigano ikitoa ripoti za waasi wanaojihami kuzunguka mji mkuu Tripoli huku serikali zinazopingana zikiwania madaraka.

Mivutano imetanda tangu bunge lenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo kumwapisha Waziri Mkuu mapema mwezi huu ikiwa ni changamoto kwa Waziri Mkuu wa muda Abdulhamid Dbeibah.

Dbeibah ambaye amekataa kukabidhi madaraka kwa Fathi Bashagha, waziri wa zamani wa mambo ya ndani aliyetajwa na bunge kama waziri mkuu, na anasema yeye ndie msimamizi halali wan chi hadi uchaguzi ufanyike.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSML) ulielezea wasiwasi wake kwenye twitter kuhusu ripoti ya uhamasishaji wa vikosi na harakati za misafara mikubwa ya makundi yenye silaha ambayo yameongeza mvutano ndani na kuzunguka Tripoli, Stephanie Williams mshauri maalum kwa Libya wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ambaye amekuwa akijaribu kuzipatanisha pande hizo mbili. “Ninawasihi kujizuia na ni muhimu kujiepusha na vitendo vya uchokozi, kwa maneno na vitendo, pamoja na uhamasishaji wa nguvu” aliandika kwenye Twitter siku ya Alhamis.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG