Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:12

Kanisa katoliki huko Malawi linaishutumu serikali yao kwa rushwa


Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera

Kanisa katoliki nchini Malawi limeishutumu serikali kwa kuwa dhaifu juu ya ufisadi katika barua nadra ya ukosoaji iliyotolewa Jumapili kwenye makanisa kote nchini humo. Mamlaka inasema wamepokea barua hiyo na watachunguza masuala yaliyoelezewa.

Barua hiyo iliyoandikwa na maaskofu wa eneo hilo, inaangazia maeneo kadhaa ambayo utawala wa Rais Lazarus Chakwera umeshindwa kuyaboresha. Miongoni mwa maeneo hayo ni mapambano dhidi ya rushwa ambapo kanisa linasema kwamba serikali imeshindwa kwa kiasi kikubwa.

Inasema utawala uliopo madarakani unaongozwa na viongozi dhaifu wasio na maamuzi ambao wanashindwa kutumia mamlaka yao kuongoza nchi.

Padri Henry Saindi, ni katibu mkuu wa baraza la maaskofu wa Malawi ambao ni umoja wa maaskofu wa kanisa katoliki nchini humo.

“Hivi karibuni ilibainika kuhusu watu ambao wenye mahusiano ya kisiasa kushiriki katika uporaji wa rasilimali za umma kwa msaada wa baadhi ya watumishi wa umma”.

Maaskofu hao walisema katika barua, kuwa wana wasi-wasi kwamba rais ambaye aliendesha kampeni dhidi ya rushwa anaendelea kuwaweka mawaziri na wasaidizi wake waliohusika katika tabia hiyo.

Barua hiyo haikutaja mifano maalum, lakini mwezi Januari Rais Chakwera, alikataa kumfukuza kazi waziri mmoja katika baraza la mawaziri, kezzie Msukwa, ambaye alikamatwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo.

Maaskofu wametoa waraka huo wakati kanisa hilo likiadhimisha miaka 30 tangu lilipotoa waraka mwingine wa kiuchungaji, ambao uliisaidia Malawi kubadili mfumo wa serikali ya chama kimoja kuingia mfumo wa vyama vingi vya siasa.

XS
SM
MD
LG