Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 03, 2024 Local time: 14:01

Kamala Harris ashiriki kumbukumbu ya miaka 57 ya Bloody Sunday


Makamu Rais Marekani kamala Harris akiwa na baadhi ya wanaharakati huko Selma, Alabama
Makamu Rais Marekani kamala Harris akiwa na baadhi ya wanaharakati huko Selma, Alabama

Makamu Rais wa Marekani, Kamala Harris alilitembelea jimbo la Alabama hapo Jumapili wakati taifa linaadhimisha kipindi muhimu katika kupigania haki ya kupiga kura ziara ambayo inajiri huku juhudi za bunge za kurejesha sheria muhimu ya kihistoria ya haki ya kupiga kura ya mwaka 1965 imekwama.

Rais Joe Biden, siku ya Jumapili alirudia wito wake wa kupitishwa kwa sheria ya kupiga kura. “Vita vya nafsi ya Marekani vina pande nyingi. Haki ya kupiga kura ndio ya msingi zaidi, Biden alisema katika taarifa ya White House.

Harris alisafiri hadi Selma kwenye jimbo la Alabama kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 57 ya "Bloody Sunday" katika siku hiyo mwaka 1965 wakati wanajeshi wa serikali ya wazungu walipowashambulia waandamanaji Weusi wanaodai haki ya kupiga kura wakijaribu kuvuka daraja la Edmund Pettus.

Makamu Rais wa kwanza mwanamke Marekani, akiwa pia m-Marekani wa kwanza mwenye asili ya kiafrika na kihindi katika jukumu hilo alizungumza kwenye eneo hilo ambalo mara nyingi hujulikana kama uwanja mtakatifu katika kupigania haki za kupiga kura kwa raia walio wachache.

Wanajeshi wa serikali mnamo machi 7 mwaka 1965 waliwapiga na kuwarushia mabomu ya machozi, waandamanaji waliokusanyika kwa amani akiwemo mwanaharakati kijana wakati huo, John Lewis, ambaye baadae alikuja kuwa mbunge wa muda mrefu wa jimbo la Georgia. Picha za ghasia hizo zililishtua taifa na kusaidia kuunga mkono kupitishwa kwa sheria ya haki ya kupiga kura ya mwaka 1965.

XS
SM
MD
LG