Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 10:31

Marais 7 wa Afrika wakutana Kinshasa kutathmini amani nchini DRC


Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa marais waliohudhuria mkutano wa amani nchini DRC
Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa marais waliohudhuria mkutano wa amani nchini DRC

Marais saba wa nchi za Afrika walikusanyika mjini Kinshasa siku ya Alhamis kutathmini makubaliano ya mwaka 2013 yaliyolenga kuimarisha amani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika eneo la mashariki lililokumbwa na ghasia na eneo la maziwa makuu.

Muundo wa amani, usalama, na ushirikiano unalenga kukuza juhudi za kuleta utulivu katika kanda. Mamilioni ya watu walikufa kutokana na ghasia, magonjwa, au njaa katika vita vya Congo vya mwaka 1996 hadi 1997 na mwaka 1998 hadi 2003 katika vita vya Congo mzozo ambao ulikumba mataifa katika eneo la Afrika mashariki na kati.

Mkutano wa Kinshasa ni wa kumi katika mifululizo iliyowaleta pamoja marais wa DRC, Afrika kusini, Uganda, Angola, Jamhuri ya Congo, Burundi, na Jamhuri ya Afrika ya kati, mwanadiplomasia mmoja alisema. Mkutano huo ulitarajia kuelezea wasiwasi wake kuhusu vifaa na usaidizi mwingine kwa makundi yenye silaha ambayo bado yanaendelea kufanya harakati zake katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG