Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 14:58

China yadai kudhibiti maambukizi ya Corona kwenye michezo ya Olimpiki


Baadhi wa wachezaji kwenye michezo ya Olimpiki mjiji Beijing
Baadhi wa wachezaji kwenye michezo ya Olimpiki mjiji Beijing

China imesema Jumanne kwamba itaalika watazamaji zaidi kwenye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi inayoendelea mjini Beijing kutokana na fanaka kubwa ya kudhibiti maambukizi ya Corona kwenye eneo maalum lililotengewa michezo hiyo.

China haikuuza tiketi za kuhudhuria kwa umma kama hatua ya kuzuia kuenea kwa virusi, lakini ilalika watu kadhaa waliyohitajika kufuata masharti makali ya kuzuia maambukizi. Tangazo hilo limefanyika wakati wa hotuba kwa wanahabari wakati afisa kwenye timu inayozuia na kudhibiti maambukizi kwenye michezo hiyo, Huang Chun akisema kwamba hali iliyoko inaruhusu zaidi ya asilimia 30 ya watazamaji kwenye baadhi ya viwanja kabla ya michezo hiyo kumalizika.

Ameongeza kusema kwamba wanatathmini kuongeza watazamaji zaidi kutokana na kuwa hali imedhibitiwa kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya michezo hiyo. Taarifa zimeongeza kusema kwamba hakuna maambukizi mapya ya corona yaliyoripotiwa kwenye mji wa kusini magharibi wa Baise siku moja baada ya shughuli za kawaida kusitishwa kutokana na wimbi jipya la maambukizi.

XS
SM
MD
LG