Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:49

Rais wa Afrika Kusini amkemea vikali waziri wa utali baada ya kushambulia katiba ya nchi na mahakama


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akitoa ushahidi mbele ya kamati ya uchunguzi, Zondo Commission of Inquiry, Johannesburg, Aug 12, 2021. Picha ya Reuters.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akitoa ushahidi mbele ya kamati ya uchunguzi, Zondo Commission of Inquiry, Johannesburg, Aug 12, 2021. Picha ya Reuters.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumatatu amemkaripia waziri wa utali Lindiwe Sisulu baada ya kuishambulia katiba na kusema majaji wana kasumba za kikoloni, matamshi makali ambayo yamechochea uvumi kuhusu mvutano ndani ya chama tawala. 

Bi Sisulu ni binti wa wanaharaki mashuhuri wa kupinga ubaguzi wa rangi, Walter na Albertina Sisulu, alianzisha mashambulizi yake yasiyokuwa ya kawaida dhidi ya mahakama na katiba katika maoni yaliyochapishwa kwenye tovuti huru ya habari( IOL) siku za hivi karibuni.

Waziri huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 67 aliwakashifu majaji wakuu ambao hakuwataja majina kuwa ni “ Waafrika waliotawaliwa kiakili” ambao wanafurahia tu kulamba mate ya wale wanaodai ubora kwa kusema uongo.

Pia alishambulia katiba ya Afrika Kusini iliyoandaliwa baada ya enzi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, akisema kuwa imeshindwa kuboresha maisha ya watu wengi weusi wa Afrika Kusini ambao bado wanaishi katika umaskini.

Matamshi yake ambayo yalizua mjadala mkali, yalichochea uvumi kwamba Sisulu anapanga kugombea uongozi wa chama tawala cha African National Congress katika mkutano wa mwezi Disemba.

Ramaphosa alijibu kile alichoita “mashambulizi dhidi ya uhuru na uadilifu wa mahakama yetu” katika jarida lake la kila wiki leo Jumatatu.

“Lazima tupambane dhidi ya juhudi zozote ambazo zinataka kuhujumu demokrasia yetu iliyopatikana kwa bidii”, Ramaphosa ameandika.

XS
SM
MD
LG