Idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali ya meli ya kubeba mizigo kaskazini mashariki mwa Madagascar imefikia watu 83.
Hali mbaya ya hewa ambayo imepelekea baharikuchafuka imepelekea juhudi za kutafuta watu watano ambao hawajulikani walipo, kusitishwa.
Meli hiyo ambayo ilikuwa imebeba watu kinyume cha sheria, ilikuwa imebeba uzito kuzidi kiasi.
Maji alijaa kwenye injini ya Meli hiyo kabla ya kuzama, Jumatatu.
Watu 50 walinusurika , na shughuli ya kuwatafuta watu wengine watano itaendelea Alhamisi.
Mojawapo ya ndege za helikopta iliyokuwa inaelekea kwenye eneo la tukio kusaidia katika uokoaji, ilianguka baharini Jumatatu.