Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 00:26

Mnada wa mali za Diego Maradona washindwa kuvutia wanunuzi


Mnada kwa njia ya mtandao wa vitu 90 vya nguli wa zamani wa soka Diego Maradona ulifanyika Jumapili, na umeshindwa kuwavutia walio ingia kwenye mnada.

Ulikuwa ukinadi nyumba yake, magari mawili ana ya BMW na nyumba ambayo aliwanunulia wazazi wake pamoja na vitu vingine lakini watu walioingia mnadani hawakuvutiwa na vitu hivyo.

Zaidi ya watu 1,500 walijiandikisha kukishiriki katika mnada kutoka Latin America, Italia, Ufaransa, Uingereza, Russia, na Dubai kwa mujibu wa waandaaji wa mnada huo.

Lakini ilipofika mwishoni mwa mnada huo uliochukuwa saa tatu, mauzo yaliyofanyika yalifikia dola 26,000 tu katika vitu vilivyokuwa na thamani ya dola milioni 1.4 kwa mujibu wa tathimini ya shirika la habari la AFP.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG