Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:16

Viongozi wa EU wanakutana kujadili Omicron


Bendera za umoja wa ulaya katika makao makuu ya umoja huo Brussels, Ubelgiji
Bendera za umoja wa ulaya katika makao makuu ya umoja huo Brussels, Ubelgiji

Viongozi wa umoja wa ulaya wanakutana alhamisi kujaribu kuweka mikakati ya kudhibithi maambukizi ya aina mpya ya virusi vya Corona – Omicron, vinavyosambaa kwa kasi katika nchi hizo.

Viongozi wanatarajiwa kujadili mikakati ya kuzuia maambukizi bila kufunga mipaka ya nchi zao.

Viongozi hao wanataka kuzuia kuweka hatua zinazogongana katika kudhibiti maambukizi, wakati huu ambapo sherehe za kuadhimisha krisimasi na mwaka mpya zinakaribia.

Wanalenga kuweka amri kwamba kila msafiri anayeingia au kutoka katika nchi hizo lazima awe na cheti cha kuonyesha kwamba amepimwa na hajaambukizwa virusi vya Corona.

Baraza la umoja wa ulaya, linalowaleta Pamoja viongozi wa umoja huo, limesema kwamba hatua zitakazochukuliwa hazistahili kuvuruga misingi ya soko huru kati ya nchi wanachama wa umoja huo.

XS
SM
MD
LG