Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:52

Chakula cha misaada chaibiwa Ethiopia


Umoja wa mataifa, Jumatano umesema kwamba kiwango kikubwa cha chakula kilichokuwa kisambazwe kimeibiwa katika maghala kaskazini Ethiopia, na kusababisha kusimamishwa kwa usambazaji wake katika miji miwili.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amewaeleza wanahabari kwamba timu ya shirika la mpango wa chakula duniani – WFP – iliyoko katika eneo hilo ilishindwa kuzuia wizi huo baada ya manyanyaso makubwa, ikiwemo wafanyakazi kushikiwa bunduki.

Amesema kutokana na hilo WFP imesitisha usambazaji wa chakula katika miji ya Dessie na Kombolcha.

Msemaji huyo amesema wizi huo uliofanywa na kundi la watu, baadhi yao kwa kiasi fulani walikuwa kutoka vikosi vya TPLF, na baadhi walikuwa watu wa kawaida.

Miji ambako wizi umetokea ipo kaskazini mwa Ethiopia katika jimbo la Amhara.

XS
SM
MD
LG