Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:53

Instagram kuwakumbusha vijana kuchukua mapumziko endapo wanakaa kwa mtandao muda mrefu


Instagram imezindua teknolojia inayowahimiza vijana kuchukua mapumziko wanapotumia mtandao huo wa picha, na kutangaza ubunifu mwingine wenye lengo la kuwalinda vijana dhidi ya maudhui yasiyo mazuri.

Instagram, inayomilikiwa na kampuni ya Meta, ilikuwa imetangaza kwamba ubunifu huo wa kutaka mtumiaji kuchukua mapumziko, unawahimiza vijana kuacha kuutumia kama wamekuwa wakiutumia kwa muda mrefu mfululizo bila mapumziko.

Utekelezaji wake umeanza Jumanne nchini Marekani, Uingereza, Ireland, Canada, New Zealand na Australia, unatarajiwa kuzinduliwa katika nchi nyingine mwaka ujao.

Hii ni mojawapo ya hatua ambazo kampuni ya Meta imechukua kufuatia lawama kwamba haifanyi vya kutosha kukabiliana na maudhui potofu.

XS
SM
MD
LG