Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:43

Mshukiwa wa mauaji ya Jamal Khashoggi


Mshukiwa wa mauaji ya mwanahabari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi, alikamatwa Jumanne katika uwanja wa ndege nje ya jiji la Paris, kwa mujibu wa vyanzo vya mahakama, polisi, na uwanja wa ndege.

Khashoggi, mwanahabari wa Saudi Arabia, aliyekuwa uhamishoni Marekani, aliuwawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, mjini Istanbul na mwili wake kukatwa vipande vipande.

Ukamataji huo umetokea siku kadhaa baada ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kukutana uso kwa uso na mwana-mfalme Mohammed Bin Salman nchini Saudi Arabia.

Rais Macron alikuwa kiongozi wa kwanza wa taifa la magaharibi kutembelea taifa la kifalme la Saudi Arabia, toka alipouwawa mwanahabari Jamal Khashoggi Oktoba m waka 2018.

Mshukiwa huyo ametajwa kuwa ni Khaled Aedh Al-Otabi mlinzi wa zamani wa wa ufalme wa Saudi Arabia, polisi imesema.

XS
SM
MD
LG