Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:55

Uchumi ni jambo moja wapo ambalo limemrejesha waziri mkuu wa Sudan


Waziri mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok, Jumatatu amesema kwamba kuendeleza mafanikio ya kiuchumi baada ya kipindi cha miaka miwili kupita ni jambo lililomfanya arejee madarakani chini ya makubaliano na jeshi ikiwa ni takriban mwezi mmoja toka alipopinduliwa na jeshi.

Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters katika makazi yake mjini Khartoum ambapo alikuwa amewekwa kizuizini toka Oktoba 25, jeshi lilipochukuwa madaraka, Hamdok amesema kwamba anaamini katika serekali yake ya sasa na atateuwa watu ambao watakuza kiwango cha maisha ya watu.

Vyama vikuu vya kisiasa na vuguvugu lenye nguvu la Sudan lililokuwa likiandamana kwa pamoja waumepinga uamuzi wa Hamdok kutia Saini makubaliano na jeshi Jumapili huku baadhi wakiita ni usaliti ama wakisema imetoa kinga kwa mapinduzi yaliuofanywa na jeshi.

XS
SM
MD
LG