Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:59

ECOWAS kujadili mapinduzi ya kijeshi Guinea na Mali


Wanajeshi walioshiriki katika mapinduzi nchini Ghana wakishika doria wakati wa mkutano wa viongozi wa ECOWAS mjini Conakry. Sept 17 2021
Wanajeshi walioshiriki katika mapinduzi nchini Ghana wakishika doria wakati wa mkutano wa viongozi wa ECOWAS mjini Conakry. Sept 17 2021

Mabalozi wa nchi za jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS wamekutana na Waziri wa mambo ya nje wa Guinea mjini Conarky, kabla ya kufanyika kongamano la jumuiya hiyo litakalofanyika jumapili kujadili hali ya usalama nchini Guinea na Mali.

Jumuiya hiyo imesitisha uanachama wa Guinea na kutaka viongozi wa mapinduzi kuachilia huru rais Alpha Conde.

Viongozi wa mapinduzi ya kijeshi wametakiwa pia kuandaa uchaguzi mkuu na kurejesha utawala wa kikatiba nchini Guinea.

Col. Mamady Doumbouya – ambaye aliongoza mapinduzi hayo, aliapishwa kama rais wa serikali ya mpito mwezi Oktoba, na kubuni baraza lake la mawaziri, na kuunda serikali ya inayoongoza nchi hiyo katika kurejesha utawala wa kiraia.

Wanajeshi walipindua serikali yar ais Alpha Conde, ambaye aligombea mhula wa tatu madarakani baada ya kubadilisha katiba.

XS
SM
MD
LG