Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 08:53

Magavana wanaopinga chanjo kwa lazima kushitaki serikali


Rais wa Marekani Joe Biden akijitayarisha kuzungumzia kuhusu chanjo dhidi ya Corona kwa watoto.

Magavana wa chama cha Republican wanatarajiwa kuishitaki serikali kuu ya Marekani hii leo kukomesha utawala wa rais Joe Biden kutekeleza amri ya kutaka wafanyakazi wa serikali kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona kwa lazima.

Magavana hao wanasema amri hiyo inavunja uhuru wa watu.

Gavana wa Florida Ron DeSantis, amesema kwamba ataungana na magavana wa Georgia na Alabama katika kesi dhidi ya utawala wa Biden, kupinga amari hiyo itakayoanza kutekelezwa Januari tarehe 4.

Ron DeSantis, amesema kwamba serikali haiwezi kulazimisha sera ya kimatibabu kwa watu kwa kudai kwamba inatekeleza masharti ya kikazi.

Magavana wa Indiana, Iowa na Nebraska nao wametangaza kupinga sera hiyo mahakamani.

Gavana wa Texas Ken Paxton ambaye pia ni mrepublican, ametangaza kushitaki mahakamani sera hiyo ya serikali kuu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG