Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 15:53

Jeshi la Ethiopia lafanya mashambulizi zaidi Tigray


Jeshi la Ethiopia Jumapili lilizindua mashambulizi mawili ya anga katika kile afisa wa serekali amesema yamelenga sehemu muhimu zinazo shikiliwa na Wa-Tigray.

Shambulizi hilo limefanya kuwa wiki ya mashambulizi yanayofanywa takriban kila siku katika jimbo la kaskazini.

Mashambulizi yanafanyika mbali ya mji mkuu wa Mekele, na kutoa ishara kwamba kuna uwezekano wa jeshi kusambaza kampeni ya mashambulizi ya anga.

Mpaka sasa mashambulizi yamepingwa na jumuiya ya kimataifa, na kusimamisha safari za ndege za Umoja wa Mataifa kwenye sehemu yenye tishio la baa la njaa.

Msemaji wa serekali ya Ethiopia, Selamawit Kassa, amesema kwamba Jumapili eneo la magharibi la Mai Sebri ambalo lilitumika kama kambi ya mafunzo ya TPLF, na komandi yao ya kijeshi lililengwa na shambulizi la anga

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG