Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 10:29

Uchunguzi wa maoni waonyesha Rais Joe Biden anaungwa mkono na raia wengi wa Marekani


Rais wa Marekani, Joe Biden

Wamarekani wengi wanafurahishwa na utawala wa rais wao Joe Biden, akiwa anakaribia kumaliza siku zake za 100 za mwanzo, kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni wa taasisi mbili.

Wengi wao wametoa maoni ya kumuunga mkono katika namna alivyo shughulikia janga la virusi vya corona, lakini hawafurahishwi na namna alivyo shughulikia kundi la wahamiaji katika mpaka na Mexico.

Uchunguzi wa maoni wa gazeti la Washington Post, na ABC, unaonyesha asilimia 52 ya watu wazima wanamuunga mkono ikilinganishwa na asilimia 42 ambao hawamuungi mkono.

Uchunguzi wote wa maoni unaonyesha kuwa hali ya mgawanyiko wa kisiasa wa nchini haujabadilika toka uchaguzi wa mwaka 2020 ambao rais Baiden alimshinda aliyekuwa rais wakati huo Donald Trump.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG