Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 15:09

Uchaguzi kuitishwa Algeria


Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune Alhamisi amesaini sheria inayoitisha uchaguzi wa awali wa bunge tarehe 12 June baada ya kulivunja bunge mwezi uliyopita.

Uchaguzi wa bunge ulikua umepangwa kufanyika mwaka wa 2022, lakini mwezi Februari rais Tebboune alilivunja bunge na kuomba uchaguzi mwengine ufanyike kabla ya mwaka huu kama sehemu ya mageuzi.

Tebboune aliachia huru darzeni ya wanaharakati wanaotetea demokrasia wa vuguvugu la Hirak lililoanda maandamano ya mabadiliko, ambalo lilimlazimisha mtangulizi wake Abdelaziz Boutlefika kujiuzulu mwaka wa 2019.

Uchaguzi unaokuja wa bunge utafanyika chini ya sheria mpya ya uchaguzi, ambayo iliidhinishwa na rais Tebboune, taarifa kutoka ofisi yake imesema.

Mwezi uliopita, Tebboune aliahidi kuwa uchaguzi hautakuwa na ufisadi, na utafungua milango ya bunge kwa vijana, akiongeza kuwa lazima vijana wawe na uzito wa kisiasa.

Maandamano yalionekana kama mwamko kukiwa na maandamano mengine kote nchini, baada ya kusitishwa mwaka jana kufuatia masharti ya kupambana na janga la corona.

Waandamanaji wanaomba mabadiliko kamili ya mfumo wa uongozi uliopo tangu Algeria ijitapitie uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka wa 1962, n kumalizika kwa ushawishi wa jeshi katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG