Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:43

Mkataba wa Uingereza kuondoka umoja wa ulaya wapatikana


Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Uingereza imekubaliana na umoja wa ulaya kuhusu mkataba mpya wa kibiashara, zaidi ya miaka minne baada ya Uingereza kupiga kura kujiondoa umoja huo.

Mkataba wa leo unanusuru Uingereza na umoja wa ulaya kuingia katika hali ya mgogoro endapo haungepatikana kufikia mwishoni mwa mwezi huu.

Mkuu wa tume ya umoja wa ulaya Ursula Von der Leyen, ametaja mkataba huo kuwa mzuri.

Uingereza ilijiondoa kuwa mwanachama kamili wa umoja wa ulaya mwezi Januari, kufuatia kura ya maamuzi iliyofanyika nchini humo Juni tarehe 23 2016.

Hata hivyo, ilikubali kuendelea kuwa katika umoja huo hadi mwishoni mwa mwaka 2020 ili kufanya majadiliano ya kuweka mazingira mema ya kufanya biashara na nchi 27, wanachama wa umoja huo.

Makubaliano ya biashara yaliyopatikana hii leo yanahitajika kuidhinishwa na bunge la ulaya ndani ya wiki chache zijazo.

Mkataba huo utatoa fursa ya kuwepo ushuru wa kiwango cha chini na gharama ya chini kwa bidhaa zinazotoka Uingereza, vitu ambavyo havingekuwepo endapo Uingereza ingeondoka umoja huo bila mkataba wa biashara.

Mkataba huo sasa unakamilisha mchakato wa zaidi ya miaka 4 ambao kwa wakati mmoja ulionekana kama mgumu kufanikiwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanachama wa umoja wa ulaya kuondoka rasmi umoja huo.

XS
SM
MD
LG