Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 15:36

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak atapewa maziko ya kijeshi


Hosni Mubarak akiwapungia mkono wafuasi wake kutoka chumba chake cha hospitali April 16, 2016
Hosni Mubarak akiwapungia mkono wafuasi wake kutoka chumba chake cha hospitali April 16, 2016

Rais wa zamani wa muda mrefu wa Misri amefariki akiwa na umri wa miaka 91 katika hospitali ya kijeshi ya Galaa mjini Cairo.

Shemeji yake Mubarak, Jenerali Mounir Thabet amesema Jumanne kwamba familia yake ilikua hospitali pamoja nae alipofariki na ofisi ya rais itapanga mazishi yake.

Mubarak aliyekua kiongozi mwenye nguvu na alama ya utulivu mashariki ya kati aliondolewa madarakani 2011 kutokana na mapinduzi ya wananchi.

Kiongozi huyo wa zamani Hosni Mubarak alikua madarakani kwa miaka 30 na sawa na viongozi wengine wa nchi za kiarabu wakati huo aliligeuza taifa hilo kuwa sawa na himaya yake binafsi.

Hosni Mubara akiwa pamoja na waziri mkuu wa Israel Shimon Peres
Hosni Mubara akiwa pamoja na waziri mkuu wa Israel Shimon Peres

Aliwaweka marafiki na familia katika nafasi za juu za madaraka, na ilionekana alikua anamtayarisha kijana wake kuchukua nafasi yake.

Mubarak alizaliwa mwaka 1928 na kujiunga na jeshi akiwa kijana na kupanda vyeo mbali mbali kwa haraka hadi kua mkuu wa jeshi la anga. Alipata umashuri alilipongoza nchi yake katika vita kati ya Warabu na Israel 1973, na kuteuliwa kua makamu rais baada ya vita hivyo.

Akiwa makamu rais alikua kando ya rais wa zamani Anwar Sadat aliyeuliwa na wanamgambo wa kislamu 1981, kutokana na kutia saini mkataba wa amani na Israel.

Alipochukua madaraka ilikua vigumu kwake yeye kuendelea na mkataba huo wa amani lakini kutokana na msaada mkubwa wakifedha wa Marekani alichukua jukumu kubwa la kujaribu kutanzua mzozo kati ya Palestina na Israel na kuimarisha uhusiano na nchi za kiarabu.

Kwa upande wa kiuchumi, Mubarak alihidi mageuzi makubwa lakini umaskini na ukosefu wa ajira uliongezeka hadi mwishoalilazimika kuacha madaraka baada ya maandamano ya kipekee ya wananchi iliyodumu siku 18 hapo mwaka 2011.

Kijana akiuza mkate mjini Cairo
Kijana akiuza mkate mjini Cairo

Miezi michache baadae alionekana kizimbani mahakamani akituhumiwa kwa mauwaji ya waandamanaji 900. Alihukumiwa kifungo cha maisha lakini aliachiwa huru mwaka 2017 baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali mashtaka yake.

Mubarak alieyfariki akiwa hospitali atapewa maziko rasmi ya kijeshi lakini hakuna tarehe iliyotajwa bado.

XS
SM
MD
LG