Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 09:09

Machar apinga pendekezo la amani la Rais Kiir wa Sudan Kusini


Kiongozi wa Vuguvugu la Ukomboizi wa Wananchi wa Sudan (SPLM-IO) Riek Machar akisalimiana na rais Salva Kiir wa Sudan Kusini baada ya mkutano wa Entebbe, Uganda, Nov. 7, 2019.

Kiongozi wa upinzani wa Sudan Kusini Riek Machar amepinga pendekezo la kufikia amani lililotolewa na Rais Salva Kiir, linalohusiana na kupunguza idadi ya majimbo lakini kuunda pia maeneo matatu ya utawala nchini humo.

Taarifa ya tangazo la Machar iliyotolewa Jumapili ina haribu uwezekano wote wa kutanzua mzozo kati yao na matumaini ya kumaliza vita vya miaka sita.

Rais Kiir wa alitangaza jana kwamba atarudisha mfumo wa majimbo 10 kutoka 32,na kuunda maeneo matatu ya utawala ya Pibor, Ruweng na Abyei,ikiwa ni ridha kwa moja wapo ya matakwa makuu ya upinzani.

Ingawa Machar ameunga mkono uwamuzi wa serikali kuunda majimbo kimu lakini amesema hajaridhika na suala la kuundwa maeneo matatu ya utawala ambapo Ruweng na Abyei ni muhimu ya uzalishaji mafuta.

Akizungumza mjini Juba Jumamosi baada ya kukutana na maafisa wa vyeo vya juu wa jeshi na serikali, Rais Kiir amesema “ridha tuliyotoa hivi punde ni kwa ajili ya amani na nina matumaini upinzani utajibu kwa hatua sawa”.

Machar anamtaka Kiir kutafakari upya wazo la kuunda maeneo hayo akionya maeneo hayo yanaweza kuzusha matatizo zaidi.

Suala la idadi ya majimbo lina zusha utata kwa sababu mipaka yake ndio itaamua namna ya kugawanya madaraka nchini humo.

Kiir na kiongozi wa waasi Machar anaeishi uhamishoni, wanakabiliwa na shikikizo la kimataifa kutanzua tofauti kati yao ifikapo Februari 22 na kuunda serikali ya umoja kama sehemu ya makubaliano ya amani.

Tayari wameshindwa mara mbili kutekeleza makubaliano kwa muda ulowekwa ili kuweza kumaliza vita vya miaka sita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo sababisha vifo vya watu 380,000 na mamilioni kuwa katika hali ya umaskini kabisa au kupoteza makazi yao.

Kiir na Machar walikutana Ethopia mapema mwezi Februari, lakini mazungumzo yalimalizika bila kufikia makubaliano.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG