Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 20:33

Rais Museveni asema hana haraka ya kustaafu


President Yoweri Kaguta Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hana haraka ya kustaafu, na wala hana mpango wa kumwandaa mtu yeyote kurithi nafasi yake na badala yake anazingatia kuimarisha ukuaji wa Uganda na bara la Afrika kwa jumla.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hana haraka ya kustaafu, na wala hana mpango wa kumwandaa mtu yeyote kurithi nafasi yake na badala yake anazingatia kuimarisha ukuaji wa Uganda na bara la Afrika kwa jumla.

Katika mawasiliano ya moja kwa moja na wafuasi wake kwenye mtandao wa kijamii wa facebook, Museveni amesema viongozi walio madarakani katika bara la Afrika, hawajaonyesha nia ya dhati kusuluhisha matatizo yanayolikumba bara hilo, na hivyo hawezi kuwa mwenye amani endapo atastaafu hii leo.

Museveni awasiliano na wafuasi wake kwa facebook akiwa katika ndege

Wakati alikuwa safarini kutoka Uganda hadi Yokohama, Japan, rais wa Uganda Yowweri Museveni alitumia mda huo kuwasiliana na wafuasi wake kwenye mtandao wa kijamii, anaowaita kuwa wajukuu wake.

Wajukuu walimuuliza Museveni maswali mengi kuhusu hali ya Uganda, yanayowakera na yanayowafurahisha, wakiangazia maswala ya demokrasia, uchumi, na hali yao ya maisha.

Vijana waahidi Museveni kumfanya baba wa taifa

Lakini lililoangaziwa Zaidi ni kuhusu utawala wa miaka 33 wa Museveni ambao wajukuu wake wanasema, umetosha, na anastahili kustaafu ili kuwaachia vijana kuongoza nchi.

Wafuasi wa museveni kwenye mtandao wa kijamii wa facebook, wanamtaka astaafu na awe mshauri, wakipendekeza kwamba mbunge Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, awe mrithi wake, wakiahidi kumtambua Museveni kama baba wa taifa na kumpa heshima za kitaifa.

Lakini Museveni, amechukua mda mrefu kujibu hoja hiyo akisema hana mipango ya kustaafu kwa sasa wala kumwandaa mrithi wake.

Museveni amesema ana kazi nyingi sana iliyosalia kwake kutimiza kwa manufaa ya Uganda, jumuiya ya Afrika mashariki, Maziwa makuu na bara la Afrika kwa jumla.

Maoni ya wachambuzi

Wachambuzi kama Francis Babu, wanasema Museveni ametuma ujumbe kwamba si wakuondoka madarakani kwa sasa.

“kitu kimoja nimeona Uganda ni kwamba kila mtu anataka awe rais, jambo ambalo haliwezikani. Museveni naye anataka aendelee kuwa pale. Sasa, inategemea na chama chake. Kama chama kinataka aendelee kuwa rais, sasa ni jukumu la wapiga kura kuamua” amesema Francis Babu.

Vile vile, Museveni mwenye umri wa miaka 75, anataka vijana, akiwemo Bobi Wine, kumuunga mkono katika ndoto yake kubwa ya kuhakikisha bara la Afrika lililoendelea kabisa kiuchumi katika siku za usoni.

Museveni amesisitiza kwamba Uganda na bara la Afrika kwa jumla, halina mtu mwenye uwezo wa kutimiza ndoto kubwa aliyo nayo, ya kuimarisha maendeleo ya uchumi, demokrasia na maisha bora kwa kila mtu. Lakini Samuel Kisitu, mchambuzi wa siasa za Uganda, ana mtazamo tofauti.

“Rais Museveni ni mtu ambaye hamwamini mtu yeyote kabisa hata ukiangalia wale ambao amefanya nao kazi, kuna jinsi anawashusha heshima na kuwadhalilisha waonekana kama watu ambao hawana uwezo wa kuongoza nchi na kila kinachofanyika ni juhudi zake pekee yake. Hii ndio sababu anasema kwamba ni yeye pekee ana maono ya nchi, jumuiya ya Afrika mashariki na hata Afrika nzima” ameeleza Kisitu.

Kitendawili cha Museveni kustaafu

Museveni, ameahirisha ahadi yake ya kustaafu mara kadhaa katika kipindi cha miaka 33 iliyopita ambayo amekuwa madarakani.

Katika chaguzi za 1995, 2001 na 2006, Museveni aliahidi kwamba angestaafu, lakini kila mara baada ya kuchaguliwa, huanza mchakato mpya kuondoa vizuizi vinaweza kumzuia kugombea mhula mwingine tena.

Kizuizi kilichokuwa kimesalia ni cha umri kwa wagombea wa urais, ambapo katiba ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2017 na kuondoa kifungo hicho.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG