Benki kuu ya Uganda imeongeza kiwango cha riba kwa benki za biashara kwa kiasi cha asilimia 10, ikiwa ongezeko la juu Zaidi kwa mda wa miaka mitatu, na kuzua hofu kwamba huenda nci hiyo ikakumbwa na mfuko wa juu wa gharama ya maisha.
Gavana wa benki kuu ya Uganda Prof Emmanuel Tmusiime Mutebile, ameambia waandishi wa habari kwamba mfumuko wa fedha unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 5 zaidi katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Mchambuzi wa maswala ya uchumi nchini Uganda - Razia Khan- amesema kwamba hatua ya benki kuu kuongeza kiwango cha riba ilitarajiwa, wakati bei ya mafuta ikitarajiwa kuongezeka Zaidi kati ka historia ya nchi hiyo na kufikia shilingi 5000 kwa kila lita ya mafuta ya petrol kutoka shilingi 3500 za sasa.