Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:25

Wanawake wa Saudia wafurahia uamuzi wa kuendesha gari


Azza Al Shmasani aingia ndani ya gari lake kukaidi marufuku ya kuendesha gari mjini Riyadh
Azza Al Shmasani aingia ndani ya gari lake kukaidi marufuku ya kuendesha gari mjini Riyadh

Maoni yamegawika huko Saudi Arabia kufuatia uamuzi wa Mfalme Salman kumruhusu mwanamke kuweza kuendesha gari kuanzia mwezi June Mwakani.

Wanaharakati waandishi wa habari na watumishi wa umma pamoja na wanawake wamefurahia uwamuzi huo wengi wakisema wa kihistoria na ushindi kwa wanawake katika haki yao ya kujiamulia jinsi wanavyotaka kusafiri.

Abdallah Muawiya mwandishi habari wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio Saudi Arabia, anasema wanaharakati walioanza mapambano yao tangu mwanzoni mwa miaka 1990 wamefurahia hatua hiyo.

Wanawake wa Saudi wafurahia uwamuzi wa kuendesha gari
please wait

No media source currently available

0:00 0:09:58 0:00

"Kwa hiyo harakati zao hizi tunaweza kusema zimesaidia vile vile kuisukuma serikali mpaka Mfalme Salman kuweza kufikia uamuzi huu wa kuwaruhusu kina mama kuendesha magari." amesema Muawiya.

Kamati maalum imeundwa kuweka masharti na utaratibu kwa wanawake kuweza kupata liseni na kuruhusiwa kuendesha magari kuanzia mwezi June 2018.

XS
SM
MD
LG