Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:07

Mwisho wa enzi ya Hayatou CAF


Issa Hayatou rais wa CAF na kaimu katibu mkuu wa FIFA Markus Kattner
Issa Hayatou rais wa CAF na kaimu katibu mkuu wa FIFA Markus Kattner

Rais wa Shirikisho la Kandanda la Madagascar Ahmad Ahmad amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Kandanda la Africa, CAF, na hivyo kuhitimisha miaka 29 ya uongozi wa Issa Hayatou.

Ahmad alichaguliwa kwa kura 34 dhidi ya 20 alizopata Hayatou wakati wa uchaguzi uliofanyika mjini Addis Ababa siku ya Alhamisi, wakati wa mkutano mkuu wa CAF.

Hayo ni matokeo makubwa katika kandana barani Afrika kwani ni mara ya kwanza kufanyika mabadiliko makubwa tangu Mcameron Hayatou kuchukua uongozi 1988.

Ahmad mwenye umri wa miaka 57 alikuwa mchezaji na kocha kabla ya kuchukua uongozi wa shirika la kandanda la Madagascar mwaka 2003.

Aliwashangaza wajumbe wenzake wa CAF mapema mwaka huu alipoanza kuzungumzia mabadiliko katika shirikisho hilo, na mara moja kuweza kuungwa mkono na wengi ambao wamekuwa wakizungumzia jambo hilo kwa faragha.

Hayatou amesifiwa kuongeza idadi ya timu za Afrika kushiriki katika finali ya Kombe la Dunia na amepoteza nafasi yake kama makamu rais muandamizi wa Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA.

XS
SM
MD
LG