Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 04:31

Uhusiano wa Trump na Putin Bado ni Kitandawili kwa Wamarekani


Polisi Russia wawakamata wapinzani wa kisiasa katika maandamano ya kuipinga serikali
Polisi Russia wawakamata wapinzani wa kisiasa katika maandamano ya kuipinga serikali

Vikundi vya wanaharakati wa haki za binadamu, baadhi ya wabunge, majenerali wastaafu na mabalozi wa zamani wamesema wana wasiwasi juu ya kitendo cha Rais Donald Trump kuendelea kumtetea Rais Vladimir Putin.

Katika mahojiano yaliyotangazwa Jumapili na kituo cha televisheni cha Fox kabla ya mchezo maarufu wa mpira wa miguu wa marekani (Super Bowl) kuanza, Trump alirejea kusema ana mheshimu Putin.

Wakati mwandishi Bill O’Reilly alipomdadisi Trump, akimwita rais wa Russia “Muuaji” Trump alijibu: “Tunawauaji wengi. Unafikiria nini? Nchi yetu haina makosa?”

Kremlin imekitaka kituo cha Fox kiombe radhi katika kile walichokiita maoni “yasio kubalika na ya kiushari ”

Hata hivyo O’Reilly alidharau malalamiko hayo katika kipindi chake Jumatatu usiku, akisema Russia wanaweza “kuwasiliana na mimi katika mwaka wa 2023.”
Siku ya Jumanne, Trump katika ujumbe wa Twitter alinang’ania kuwa yeye hamfahamu Putin na kwamba hana mafungamano yeyote na Russia.

Trump alikataa kusema kitu chochote hasi kuhusu Putin katika kampeni yake ya uchaguzi, akirejea katika kujibu maswali kuhusu rais wa Russia kwa kusema kwamba Russia ni hazina na sio mzigo, ikiwa tu ataweza kuwa na maelewano mazuri na Putin, na viongozi wengine duniani.

Mkurugenzi mwenza wa programu ya waangalizi wa haki za binadamu( Human Rights Watch) Marekani, Maria McFarland, ameiambia VOA Jumatatu ana wasiwasi na maoni ya Trump kuhusu Russia.

Akiongea na Kituo cha televisheni cha CBS katika kipindi chake cha Jumapili “Face the Nation” Makamu wa Rais Mike Pence amekanusha tafsiri iliyokuwepo kuwa Trump alikuwa anazilinganisha Marekani na Russia.

“Kwa kifupi sikubaliani ya kuwa katika Trump kuzifananisha nchi hizi mbili kulikuwa na kuzihusisha nchi hizi mbili kimaadili.”

Alipoulizwa katika kipindi cha Jumapili ya tatu kinachojulikana kama “State of the Union” kinachoonyeshwa na CNN kuhusu maoni ya Trump, Kiongozi wa walio wengi wa Republikan katika Baraza la Seneti, Mitch McConnell amesema hakutaka kumkosoa Rais Trump kwa “kila tamko lake.” Lakini amesema Putin ni jasusi wa zamani wa KGB na kumwita ni “Mhuni tu”

XS
SM
MD
LG