Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 20:33

CAN 2017: Gabon yabanwa na Guinea Bissau 1 - 1

Pierre Emerick Aubameyang wa Gabon, kulia akisherehekea pamoja na wenzake alipopachika bao la kwanza katika finali za CAN 2017 dhidi ya Guinée-Bissau, mjini Libreville, Gabon.
Pierre Emerick Aubameyang wa Gabon, kulia akisherehekea pamoja na wenzake alipopachika bao la kwanza katika finali za CAN 2017 dhidi ya Guinée-Bissau, mjini Libreville, Gabon.

Wagabon walikua na matumaini makubwa mchuano ulipoanza nyumbani hasa baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kufungua mlago kwa bao la kwanza katika dakika ya 54 ya mchezo.

Guinea Bissau inayocheza kwa mara ya kwanza katika Kombe la Afrika baada ya miaka mingi iliweza kuwakata tamaa wenyeji katika dakika ya 90 pale Juary Soares alipoweza kuuwona wavu na kusawazisha mchezo huo.

Mashabiki kwenye uwanja wa l'Amitié mjini Libreville, Gabon, wakati wa mechi ya ufunguzi 2017
Mashabiki kwenye uwanja wa l'Amitié mjini Libreville, Gabon, wakati wa mechi ya ufunguzi 2017

mchezo huo wa ufunguzi utakaokumbukwa kwa muda mrefu kutokana na kwamba mashabiki wa Chui wa Gabon walianza kuzomea timu yao kipengele cha mwisho kilipopigwa.

Rais Ali Bongo aliyefungua rasmi michuano ya mwaka huu alikua pamoja na mwenzake wa Guinea Bissau Jose Mario Vaz akishuhudia jinsi vijana wake walivyoshindwa kuwika na kufiungua michuano hiyo kwa ushindi.

XS
SM
MD
LG