Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 16, 2025 Local time: 19:25

Wanajeshi wafikia makubaliano na serikali ya Ivory Coast


Wanajeshi waloasi wanafika kukutana na waziri wa ulinzi Alain-Richard Donwahi kwa mazungumzo mjini Bouaké. Januari 7 2017.
Wanajeshi waloasi wanafika kukutana na waziri wa ulinzi Alain-Richard Donwahi kwa mazungumzo mjini Bouaké. Januari 7 2017.

Ujumbe wa serikali ya Ivory Coast ukiongozwa na waziri wa ulinzi Alain-Richard Donwahi unasema umefikiamakbaliano siku ya jumamosi nawanajeshi waloasi katika kumaliza siku mbili ya uasi uloanza katika mji wa kaskazini wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Bouake.

Mjumbe wa wanajeshi waloasi Serjent Mamadou Kone, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba, mambo yamemalizika, wanajeshi wamekubali kurudi kambini baada ya serikali kukubaliana na malalamiko yao.Wanajeshi wa Ivory Coast wakipiga doria katika kijiji cha Keibly.

Wanajeshi waloasi wachukua udhibiti wa mji wa Bouake
Wanajeshi waloasi wachukua udhibiti wa mji wa Bouake

​Wanajeshi walichukua udhibiti wa karibu miji mitano ya Ivory Coast kuanzia siku ya Ijumaa ili kudai nyongeza za mishahara, marupurupu na malalamiko mengine.

Ghasia na milio ya bunduki iliripotiwa tena katika kambi kadhaa za kijeshi kote nchini usiku wa Ijuma kuamkia Jumamosi, wakati waziri wa ulinzi alikua anakutana na viongozi wa wanajeshi katika mji wa Bouake.

Akizungumza na waandishi habari kabla ya mkutano, waziri Donwahi alisema serikali itafanya kila iwezalo kushughulikia malalamiko ya wanajeshi na kuwataka kurudi katika kambi zao.

Waziri wa ulinzi Alain Richard Donwahi akizungumza na waandishi habari mjini Bouaké, Côte d’Ivoire.
Waziri wa ulinzi Alain Richard Donwahi akizungumza na waandishi habari mjini Bouaké, Côte d’Ivoire.

Wanajeshi walionekana wakishika zamu katika mijim mbali mbali na wanajeshi wa umoja wa mataifa wanaofuatilia utekelezaji wa makubaliano ya Amani ya march 2007 walikua wanashika zamu pia katika maeneo muhimu ya nchi ili kuzuia uwasi kueneea na kua mapigano.

Rais Alassane Outtara aliyehudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais wa Ghana Nana Akufo-Addo mjini Accra Jumamosi asubuhi alirudi jioni na kuitisha kikao cha dharura cha baraza lake la mawaziri.

Hii ni mara ya kwanza kwa uasi kuzuka kote nchini tangu kumallliiizika kwa vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka 2004.

Jeshi la Ivory Coast liliundwa upya baada ya makubaliano ya Amani na ni mchanganyiko wa wapiganaji wa zamani wa uasi, wanamgambo na wanajeshi wa serikali.

Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa mjini Bouake.
Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa mjini Bouake.

Hata hivyo wengi wa wanajeshi walokua wanalalamika wiki hii ni wanachama wa makundi ya wanamgambo walokua wakifahamika kama Vikosi vipya "Forces Nouvel"

XS
SM
MD
LG