Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:59

Kerry: Suluhisho la mataifa mawili Israel na Palestina liko hatarini


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekano John Kerry akizungumza kuhusu sera ya Israel na Palestina
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekano John Kerry akizungumza kuhusu sera ya Israel na Palestina

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry Jumatano ametoa ombi la mwisho lenya azma ya kuhifadhi taswira pana ya suluhisho la kuwepo mataifa mawili ya Israel na Palestina, akitahadharisha kwamba linakabiliwa na “hatari kubwa.”

Katika hotuba yake huko wizara ya mambo ya nje, Kerry pia alitetea uamuzi wa Marekani wiki iliyopita kuzuia kura yake ya turufu wakati Baraza la Usalama lilipopitisha azimio la kulaani ujenzi wa makazi ya Israeli katika maeneo ya wa-Palestina.

Baraza la Usalama linapiga kura azimio dhidi ya ujenzi wa mkazi ya Israel
Baraza la Usalama linapiga kura azimio dhidi ya ujenzi wa mkazi ya IsraelKura iliyopigwa Umoja wa Mataifa “ ilikuwa kuhusu kulinda suluhusho la kuwepo mataifa mawili,” alisema Kerry. “ Hilo ndilo tulikuwa tunalisimamia- mustakbali wa Israeli kama taifa la Kiyahudi na serikali ya kidemokrasia.”

Viongozi wa Israeli, pamoja na wabunge wa vyama vyote viwili vya Demokrat na Republikan wameukosoa msimamo huo, wakisema Marekani imeshindwa kuitetea Israeli, ambae ni mshirika mkuu wa siku nyingi.

Lakini Kerry siku ya Jumatano alitupilia mbali shutuma hizo, akisema Israeli itaendelea kuwa ni mshirika wa karibu wa Marekani, lakini kikwazo kikubwa katika kufikia amani siku za usoni ni ujenzi wa makazi.

Waziri wa nchi za nje John Kerry akizungumza kuhusu sera Israeli-Palestinian.
Waziri wa nchi za nje John Kerry akizungumza kuhusu sera Israeli-Palestinian.

"Marafiki wanatakiwa kuambiana ukweli unaouma, na urafiki unataka pande zote kuheshimiana,” Kerry alisema, akisisitiza kuwa utawala unaelemea katika suluhisho la kuwa na taifa moja jambo ambalo “walio wengi kwa yakini hawataki.”

Wa-Israeli na wa-Palestina wanaweza kuchagua kuishi pamoja katika nchi moja, au wanaweza kujitenga katika nchi mbili, alisema Kerry.

“Lakini huu ndio ukweli wa msingi: Iwapo chaguo ni nchi moja, Israeli inaweza kuwa ni taifa la Kiyahudi au la kidemokrasia, haiwezi kuwa yote mawili.

XS
SM
MD
LG