Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:13

Marekani yakanusha kuingilia kati uchaguzi wa Kenya


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na Balozi Robert Godec wakutana na wawakilishi wa asasi za kiraia mjini Nairobi
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na Balozi Robert Godec wakutana na wawakilishi wa asasi za kiraia mjini Nairobi

Serikali ya Marekani imekanusha vikali madai yasiokuwa na msingi yaliyotolewa hivi karibuni dhidi ya mradi wa Kusaidia Mfumo wa Uchaguzi Kenya (KEAP) na washirika wake wanaoutekeleza mradi huo. Mionbgoni mwa watekelezaji wakiuu ni Taasisi ya Kimataifa kwa ajili ya Mifumo ya Uchaguzi – IFES.

Kauli hiyo imetolewa Jumanne na Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert F. Godec katika taarifa kuhusu msaada wa Marekani kwa Uchaguzi wa Kenya mwaka 2017.

Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa idara ya Marekani ya Maendeleo ya Kimataifa USAID inatoa msaada kwa ajili ya uchaguzi chini ya Makubaliano ya Msaada wa Maendeleo na serikali ya Kenya, inayoruhusu kutolewa vibali vya kufanya kazi kwa washiriki wanaotekeleza mradi, ikiwemo taasisi ya IFES.

Taarifa hiyo imemnukuu balozi akisema: “Tumesikitishwa kwa jaribio la kukashifu juhudi za Marekani katika kuwasaidia wa-Kenya katika kuendesha uchaguzi huru, haki, salama na za kuaminika hapo mwaka 2017.”

“Msaada wetu unatokana na maombi ya serikali ya Kenya na Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi, IEBC na tumeendelea kufuata kanuni na sheria za Kenya, na unatolewa chini ya uangalizi wa Serikali ya Kenya, na USAID,” aliongeza kusema.

Wanawake walohudhuria warsha ya kuwawezesha wanawake wa Kenya kisasa
Wanawake walohudhuria warsha ya kuwawezesha wanawake wa Kenya kisasa

.IFES imesajiliwa Kenya chini ya Sheria ya Makampuni na ina nguvu ya kisheria kufanya shughuli zake nchini.

Katika tukio jingine kuhusiana na uchaguzi wa Kenya mabalozi wa mataifa ya 10 ya magharibi pamoja na Marekani nchini Kenya wamesema Jumanne kua kama wadau wa muda mrefu wa Kenya, nchi zao zitaendelea kuisaidia serikali ya Kenya na wakati wananchi wa Kenya wanaendelea kutafuta njia bora za kufikia malengo yao ya Katiba ya mwaka 2010 na Dira ya Kenya ya mwaka 2030

“Tumeahidi kuendelea kuisaidia Kenya kuendesha uchaguzi ulio wa huru, haki na wa kweli mwaka ujao, na kutoa msaada wa kitaalamu kwa taasisi za serikali na asasi za kiraia, bila ya kufungamana na chama chochote cha kisiasa,” ilieleza taarifa yao ya pamoja.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa :”Tunafanya hili kwa sababu demokrasia ya uhakika inategemea sio tu taasisi za serikali lakini pia asasi binafsi. Vyombo vya habari huru na jumuiya binafsi zenye kujitegemea vinajukumu kubwa katika demokrasia.”

XS
SM
MD
LG