Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:26

Trump akabiliwa na changamoto ya kukamilisha baraza la mawaziri


Rais mteule Donald Trump akizungumza na waandishi habari kwenye ukumbi wa jengo la Trump Tower in New York, Dec. 6, 2016.
Rais mteule Donald Trump akizungumza na waandishi habari kwenye ukumbi wa jengo la Trump Tower in New York, Dec. 6, 2016.

Nje ya Jumba la Trump katika mji wa New York katika Mtaa no 5 na Mtaa no 56, kunatokea makelele yenye hamasa hasa ukizingatia baridi iliyoghubika asubuhi wakati wafuasi wanaounga mkono kuhisabu upya kura katika majimbo matatu, wakiungana na mgombea Uraisi wa Chama cha Green Party, Jill Stein katika mkutano kushinikiza juu ya hatma ya kura sahihi, salama na za haki,

Jill Stein (kati kati), mgombea kiti cha rais wa chama cha Kijani
Jill Stein (kati kati), mgombea kiti cha rais wa chama cha Kijani

“Sisi tuko hapa kumhakikishia Donald Trump kwamba hatuna kitu cha kuogopa,” alisema Stein. “Ikiwa unaamini demokrasia, na unaamini katika ukweli wa ushindi wako, weka mikono yako chini, maliza vikwazo vya ukiritimba, acha vitisho na jiunge na Wamarekani ambao wanasisitiza demokrasia itakayo tutumikia sisi sote na uchaguzi tunazoweza kuamini.”

Wapinzani walijitokeza na kulikejeli kundi la wanaopinga matokeo ya uchaguzi kwa kelele. “Mnadai kughushi kwa kura, kilio cha mlengo wa kushoto hicho, Stein hawezi kubadilisha matokeo: Rais ndio Trump January 20, 2017” bango la mwanamke mmoja lilisema hilo.

Lakini mmoja wa wafuasi wa Stein alipiga kelele mnaota.

Wakati huo huo Jaji mmoja ameagiza kuhisabiwa kura mara moja katika jimbo la Michigan, moja ya majimbo muhimu yaliyokua na ushindani mkali wakati wa uchaguzi ambalo Stein anadai kwamba kura ziliibiwa kutokana na mashine za kupigia kura zilizokuwa chakavu. Hali kadhalika anashinikiza kwa mahakama ya kitaifa kutoa amri ya kura kuhisabia tena katika jimbo la Pennsylvania.

Lakini bado wengi wanafikiria kuwa juhudi za Stein katika kupigania kura kuhisabiwa tena ni upotevu wa fedha and muda. Lakini sisi kama wapiga kura tunalazimika kuhakikisha kuwa demokrasi haizuiliwi na kura zetu zinahisabia sawa sawa,” alisema Rachel Desario, ambae ni mfuasi wa Clinton aliyejumuika katika maandamano hayo siku ya Jumatatu.

Uteuzi wa Baraza la Mawaziri unaendelea

.Ndani ya Jumba la Trump, Raisi mteule aliendelea mchakato wa kuunda serikali yake.

Dkt. Ben Carson, akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Warepublican
Dkt. Ben Carson, akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Warepublican

Siku ya Jumatatu, alimchagua mmoja wa wapinzani wake katika Chama cha Republican, Daktari Bingwa mstaafu, Ben Carson kuwa ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Miji.

Trump alisema kwamba: “ Carson ni mahiri na mwenye shauku katika kuimarisha jamii na familia. Tumezungumza kwa kirefu juu ya kufufua agenda ya miji and wito wetu wa kufufua uchumi tukijikita katika maeneo ya mijini.”

Carson 65, hata hivyo hana utaalamu katika mambo ya makazi lakini alitumia sehemu ya maisha yake ya utotoni akiishi kwenye nyumba za uma, ambazo zinasimamiwa na Idara ya Nyumba and Maendeleo ya Miji.

Huko nyuma alikuwa akipinga program za serikali ambazo zilionekana kwake zikishajiisha tegemezi na siku zote amesimama kidete kuhimiza maadili ya mtu kutumia juhudi zake kupata mafanikio.

Lakini Nancy Pelosi, Kiongozi wa Kambi ya Demcrats walio wachache katika Baraza la Wawakilishi amelaumu uteuzi wa Carson na kusema ni wenye kuudhi kwa kuwa hana sifa za kazi hiyo. Lakini majina zaidi ya nyadhifa mbalimbali katika Baraza la Mawaziri yataendelea kutolewa na Rais Trump, alisema msemaji wake.

Chaguo la mwanadiplomasia wa nyadhifa ya juu latanua wigo

Makamu wa Rais Mteule Mike Pence hata hivyo baada ya kuwapuuza waandishi wa habari kuhusu uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Nje alipokuwa anaingia kwenye Jumba la Trump, alimpogenza Rais kwa spidi na msimamo imarakatika kuliunda baraza la mawaziri. Aliongeza kusema wamarekani wamepewa moyo na kuvutiwa na maamuzi ya Rais.

Trump bado anapima chaguo lake la Waziri wa Mambo ya Nje, ambayo ni nyadhifa ya juu ya mahusiano ya kimataifa, lakini wasaidizi wake wamesema chaguo hilo litafanyika wiki ijayo. Katika majina mashuhuri yaliyotajwa kama wenye uwezekano mkubwa wa kuchukua nafasi hiyo ni pamoja na aliyekuwa meya wa New York Rudy Giuliani, Mgombea wa Uraisi kwa Tiketi ya Chama cha Republican 2012, Mitt Romney, aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani, David Petraeus na Seneta wa Jimbo la Tennessee Bob Corker.

Trump azungumzia mabadiliko ya hali ya hewa

Hivi karibuni Trump pia alikutana na aliyekuwa makamu wa rais wa chama cha Democrat, Al Gore ambaye alisema alikuwa na mazungumzo marefu na yenye tija alipokutana na Rais Trump.

Makamu rais wa zamani Al Gore akizungumza na waandishi habariNew York, Dec. 5, 2016.
Makamu rais wa zamani Al Gore akizungumza na waandishi habariNew York, Dec. 5, 2016.

Gore ni mtetezi wa kimataifa kwenye kudhibiti athari za kibinadamu kwenye Mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo aliyaeleza mazungumzo yao ni kutafuta muafaka wa kweli.

“Nimegundua kuwa mazungumzo yalikuwa ya busara, na yataendelea na nitaachia hapo leo,” alisema Gore.

Aliyekuwa makamo wa rais Al Gore akizungumza na wanahabari mara baada ya kukutana na Ivanka Trump and Rais Mteule Donald Trump Katika Jumba la Trump, New York, Dec. 5, 2016.

Kadhalika Trump ameliita suala zima la mabadiliko ya hali ya hewalinalotokana na matendo ya binadamu ni Kichekesho, lakini hivi karibuni alisema yeye yuko tayari na uamuzi wa Marekani kuafiki Mkataba wa Tabia Nchi uliopitishwa Ufaransa ambao umeanza kazi mwezi uliopita.

XS
SM
MD
LG