Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:30

Clinton akubali kushindwa na Trump


Donald Trump na mgombea mwenza wake Mike Pence
Donald Trump na mgombea mwenza wake Mike Pence

Mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik Hillary Clinton, amempigia simu mpinzani wake Donald Trump wa chama cha Republican kukubali kushindwa katika uchaguzi wa rais.

Mapema usiku wa Jumanne mwenyekiti wa kampeni ya Clinton, John Podesta aliwataka mamia ya mashabiki walokusanyika katika ukumbi mjini New York kurudi nyumbani na kwamba mgombea wao hatazungumza.

Muda mfupi baadae mgombea mwenza wa chama wa Trump Mike Pence amewashukuru wafuasi na kumkaribisha rais mteule wa 45 wa marekani. Hii ikiwa ni tukio la kihistoria Marekani kwa mtu ambae hajawahi kushika nafasi au wadhifa wowote wa serikali kuchaguliwa kuliongoza taifa kuu la dunia.

Trump akiwahutubia wafuasi hao huko New York amesema Hillary amermpigia simu na kumpongeza. Mfanyabiashara huyo ametoa wito kwas wamarekani wa pande zote kuungana na kufanya kazi pamoja.

XS
SM
MD
LG