Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:22

Jamii ya Makonde watembea hadi Nairobi kudai haki zao


Jamii ya Wamakonde Kenya waandamana hadi Nairobi
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:12 0:00

Zaidi ya wakazi 300 wa jamii ya Wamakonde kutoka Pwani ya Kenya na Wapemba wanaoishi katika kaunti ya Kwale, waliwasili mjini Nairobi siku ya Alhamisi baada ya kutembea karibu km 500 kwa siku nne kutoka Kinandoni, Kwale ili kuwasilisha madai yao ya kutambuliwa kama raia wa Kenya.

Hata hivyo kati kati ya njia walisaidiwa na tume ya haki za binadam ya Kenya kwa mabasi ili kukamilisha safari yao.

Jamii ya wamakonde waandamana hadi Nairobi
Jamii ya wamakonde waandamana hadi Nairobi

Wamakonde wanasema wamesubiri kwa muda mrefu sana kupata vitambulisho baada ya kuletwa nchini humo kutoka Msumbiji na wakoloni ili kufanya kazi katika mashamba ya makongwe.

Kwa uapnde mwengine wakazi kutoka Pemba, Zanzibar, pia waliletwa na wakoloni kufanya kazi katika wilaya hiyo. Mwenyekiti wa jamii ya Makonde Thomas Nguli, anasema “ serikali ya Kenya haijatutambua hadi sasa, na ukiangalia maisha yetu tuko katika kiza, tumewekwa katika boxi. Kwa sababu kama umekosa kitambulisho umekosa kupata hati ya kuzaliwa, ukiwa huna kitambulisho umekosa kuweka pesa benki, na zaidi huwezi kusafiri nje ya nchi.”

Wakiwa njiani maafisa wa usalama waliwasimamisha mjini Voi na kuwarai kurudi wakiwahakikishia szuala lao litahadiloiwa kwenye kikao kijacho cha baraza la mawaziri. Lakini walikataa.

Wakazi wa jamii ya Makonde Kenya wawasili Nairobi
Wakazi wa jamii ya Makonde Kenya wawasili Nairobi

Inaripotiwa kwamba serikali ilijaribu mara tatu kuwaorodhesha wakazi wa jamii hizo na mara ya mwisho ilikua 2015, lakini hadi hii leo hawajapewa vyeti vya utambulisho.

Matumaini yao ni kuweza kukutana na Rais Uhuru Kenyatta na kumeleza kadhia yao.

XS
SM
MD
LG