Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 14:01

Wanawake 3 washambulia kituo cha polisi Mombasa


Wanawake 3 washambulia kituo cha polisi Mombasa
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:56 0:00

Wanawake watatu wakiwa wameva buibui wakidai wameibiwa simu zao walikwenda katika kituo kikuu cha polisi mjini Mombasa, Kenya ili kuripoti kisa hicho.

Kufuatana na mkuu wa p[olisi wa Mombasa Patterson Maelo, walipokua wanahojiwa na polisi, mmoja kati yao alitoa kisuna kumshambulia afisa wa polisi na wengine kuwarushia maafisa mabomu ya chupa ya mafuta.

Maafisa wengine walijibu shambulio hilo na kuwauwa wanawake hao watatu.
Kamanda Maelo anasemakituo kiliwaka moto na maafisa wawili wapolisi walijeruhiwa na wamelazwa hosopitali.

“Kituo kilishika moto na polisi walijibu wa kuwashambulia kwa risasi wanawake hao na kuwaua. Maafisa wawili wamejeruhiwa.” Alisema Maleo

Kamanda wa polisi hakutoa maelezo zaidi wala kusema ni kundi gani au watu wanaodhani kuhusika na shambulizi hilo.

Kikosi maalum cha bomu kilipelekwa kutengua milipuko iliyogunduliwa kwenye mili ya washambulizi hao.

XS
SM
MD
LG