Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:28

Somalia yasimamisha safari za miraa


Vijana wakitumia miraa mjini Mogadishu, 2014.
Vijana wakitumia miraa mjini Mogadishu, 2014.

Serikali ya Somalia inasema imesimamisha safari zote za ndege zinazobeba miraa kutoka Kenya kwenda Somalia kwa sababu za maslahi ya kitaifa, maafisa wanasema.

Katika mahojiano na Idhaa ya Kisomali ya VOA, Waziri wa safari za anga wa Somalia, Ali Ahmed Jangali, amesema wamechukua hatua hiyo kutokana na "maslahi ya kitaifa." Alikataa kufafanua sababu hizo.

"Ni hatua ya muda na tumeifanya kwa sababu kadha zinazohusiana na maslahi ya kitaifa," alisema Jangali. "Siko tayari kutoa maelezo zaidi."

Kenya ndio nchi inayotumiwa katika safari za kimataifa kuingia Somalia, na mahali ambapo usafirishaji mwingi wa miraa unaanzia. Inakisiwa kuna safari 20 za ndege kwa wiki kutoka Nairobi kwenda Somalia zikiwa zimebeba miraa.

Wafanyabiashara wa miraa wanakisia kuwa kiasi cha tani 20 za miraa zinaingia Somalia kutoka Kenya kila siku.

VOA inaendelea kuwatafuta maafisa wa Kenya kuhusu habari hii.

XS
SM
MD
LG