Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 03:41

Majaji wataka barua pepe mpya za Clinton kuchunguzwa


Mkurugenzi wa FBI, James Comey

Majaji wa Marekani, Jumatatu wameitaka wizara ya mambo ya njie ya Marekani kupitia barua pepe mpya za Bi Hillary Clinton, kuona kama zinaweza kuwekwa hadharani.

Shauri hilo limekuja baada ya kubainika kuwepo karibu barua pepe nyingine 15,000 za kipindi cha miaka minne ambacho mgombea urais wa Demokrat, Bi Hillary Clinton, alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Wanasheria wake awali hawakuweka wazi kuwepo kwa barua pepe hizo ambazo hazijulikani kama zinauhusiano na wizara ya mambo ya nje ama zilikuwa ni binafsi.

Vilevile haujulikani kama baadhi yake tayari zimeshatolewa kama sehemu ya barua pepe 30,000 ambazo tayari zimeshawekwa hadharani.

Barua pepe mpya ziligunduliwa na idara ya upelelezi ya Marekani FBI wakati wa uchunguzi wake wa mwaka mmoja wa matumizi ya Bi Clinton ya kituo binafsi cha kuhifadhia mawasiliano yake kilichopo New York badala ya kutumia mfumo wa serekali ambao una-ulinzi zaidi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG