Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:18

Maandamano yaishinikiza serikali ya Nigeria


Mamia ya watu nchini Nigeria waliandamana Jumatatu kuelekea makazi ya rais katika mji mkuu Abuja kuitaka serekali iwajibike zaidi kuwaokoa wasichana zaidi ya 200 waliotekwa mwaka 2014.

Maandamano hayo yamefanyika wiki moja baada ya wanamgambo wa kundi la Boko Haram kutoa kanda mpya ya video inayo onyesha zaidi ya wasichana 50 iliowateka.

Kundi hilo la wanamgambo limesema wasichana kadhaa wamefariki dunia na kutaka kubadilishana wafungwa na wasichana hao waliosalia.

Mama wa mmoja wa wasichana aliyetekwa, Esther Yakubu amesema waandamanaji wamechoshwa na juhudi za kila mara za kuitaka serekali iwaokoe wasichana hao.

Mwanamke huyo ni mama wa msichana ambaye alionekana katika mkanda wa video ulioonyeshwa na kundi hilo.

XS
SM
MD
LG