Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 09:34

Upinzani wadhibiti serikali ya Johannesburg, Afrika Kusini


Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini kimeshinda udhibiti wa serekali za mitaa kwa mara ya kwanza toka kumalizika kwa ubaguzi wa rangi katika jiji la Johannesburg, ambalo ni kitovu cha uchumi wa nchi.

Mgombea wa chama cha Democratic Allience ameshinda nafasi ya umeya katika uchaguzi wa madiwani kufuatia kushindwa kwa chama tawala cha African National Congress (ANC) katika uchaguzi wa manispaa wa Agosti 3 mwaka huu.

Huo ni moja ya ushindi wa chama cha Democratic Alliance katika maeneo ya mijini ikijumuisha kuchukuwa utawala katika mji mkuu wa Pretoria katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Hali hiyo inaashiria kubadilika kwa hali ya kisiasa nchini Afrika Kusini, ambapo chama cha ANC kimekuwa hakikabiliani na upinzani toka kuingia madarakani baada ya ubaguzi wa rangi kumalizika mwaka 1994.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG