Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 23:46

Obama: "Hakuna mwenye ujuzi kuwa rais kuliko Hillary Clinton"


Rais Barack Obama na mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik Hillary Clinton.
Rais Barack Obama na mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik Hillary Clinton.

Rais Barack Obama wa Marekani ametoa moja wapo ya hutuba za kusisimu kumunga mkono mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik Hillary Clinton wakati wa iku ya pili ya mkutano mkuu wa chama huko Philadelphia.

Amesema, "hapajakuwepo mwanamume wala mwanamke mwenye sifa na uwezo wa kua rais kuliko Hillary Clinton."

Kiongozi huyo alikua anawahutubia wajumbe wa chama cha Demokratik na taifa zima kwa ujumla juu ya uwezo na sifa za mgombea kiti wa chama cha Demokratik, akisema anafika mwisho wa utawala wake bila ya kukamilisha mengi aliyotaka kufanya na hivyo inabidi Wamarekani wamchaguwe Hillary ambae anauwezo wa kuendeleza mipango yake.

Rais Obama alifafanua nukta moja baadaa ya nyingine juu ya uwezo wa mgombea huyo aliyekua waziri wake wa mambo ya nchi za nje na kueleza kwamba anawakilisha tabaka zote za wamarekani.

President Barack Obama kwenye jukwa la mkutano wa Demokratik
President Barack Obama kwenye jukwa la mkutano wa Demokratik

"Ninawaona Wamarekani wa kila chama, kila tabak, kila imani wanaoamini kwamba tunakua na nguvu tukiwa pamoja. Weusi, weupe walatino vijana, wazee mashoga, wanaume na wanawake wenye ulemavu wote ni wazalendo wa taifa hili kuu."

Rais Obama aliwataka wamarekani wamfanyiye Clinton kile walicomfanyika mika minane iliyopita nayo ni kumchagua kua rais wa Marekani.

Kabla ya Obama kuzungumza, mgombea mwenza Time Kaine alikubali muteuzi wake na kujitambulisha kama mwanasiasa aliyeanza kuanzia daraja ya udiwani na kupanda kufikia gavana, Ssneta na sasa anamatumaini kua makamu rais.

Makamu Rais wa Marekani Joe Biden
Makamu Rais wa Marekani Joe Biden

Makamu Rais Joe Biden, pamoja na vigogo wengine wa chama hicho walikua miongoni mwa walozungumza kuwataka wanachama kuungana nyuma ya mgombea wao, ili kuweza kumshinda mpinzani wao mkuu Donald Trump.

XS
SM
MD
LG