Tajiri Donald Trump amepewa siku ya Alhamisi kua siku yake ya kunawiri atakapo kubali uteuzi wake kua mgombea kiti cha rais wa chama cha republican.
Baada ya kusifiwa kwa siku tatu na vigogo wa chama, na kuteuliwa rasmi siku ya Jumanne, Trump atahutubia mkutano mkuu wa Cleveland katika siku ya mwisho chini ya mada ya "Ifanye Marekani iwe moja."
Umoja ni jambo la kuzingatiwa miongoni mwa warepublicans kutokana na uchaguzi wa awali ulokua na ushindani na mvutano mkubwa ulopelekea kuteuliwa kwqa Trump kama mgombea wao atakae pambana na Hillary Clinton wa chama cha Democratic.
Wapinzani wa Trump, Marco Rubio, Chris Christie na Ben Carson waliacha kando tofauti zao na kutumia hotuba zao kumunga mkono. Lakini mhasimu wake mkuu Cruz , alizomewa alipojaribu kuwambia wapiga kura watumiye hisia zao kuwachagua wagombea watakaolinda maslahi yao.
Alizomewa, huku wajumbe wakimtaka atangaze uungaji mkono wake kwa Trump, jambo ambalo hakulifanya. Mjuda mfupi baadae Trump aliandika kwenye Twitter.
"Lo Cruz amezomewa akiwa jukwani,. hakutekeleza ahadi. Hamna neno, muache azungumze."
Mgombea mwenza wa Trump, Gavana wa Indiana Mike Pence, alitoa hotuba yake kuu ya kukubali uteuzi wa kua makamu rais na kujieleza kama mtu wa dini, atakae weza kuleta uwiyano katika kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Novemba.