Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 23:30

Trump ateuliwa rasmi kuwa mgombea kiti cha rais wa chama cha Republican


Wajumbe wa chama cha republican wapiga kura kumteua mgombea wao rasmi July 19, 2016.
Wajumbe wa chama cha republican wapiga kura kumteua mgombea wao rasmi July 19, 2016.

Tajiri, anayesema anachofikiria Donald Trump ameteuliwa rasmi kuwa mgombea kiti cha rais wa chama cha Republican katika uchaguzi uliofanyika katika mkutano mkuu wa chama mjini Cleveland, Ohio.

Katika utaratibu wa wajumbe wa kila jimbo kujitokeza na kutangaza kura zao wanampa nani, Trump alipata kura 1347 zinazohitajika kua mgombea wa chama hicho.

u Ujumbe wa Kansas unaonekana kwenye ukumbi ukipiga kura, July 19, 2016.
u Ujumbe wa Kansas unaonekana kwenye ukumbi ukipiga kura, July 19, 2016.

Uwamuzi huu umetokea baada ya kuwepo na shaka kwamba huwenda wajumbe wa chama hicho wakagawika na kutompa mwanabishara huyo anaegeuka kua mwanasiasa kura zao.

Huu ni uwamuzi wa kihistoria kwa chama hicho kutokana na kumteua mtu asie mwanasiasa na ambae hakua mwanachama wa dhati wa chama hicho.

Baadhi ya viongozi wa chama wamesusia mkutano huu na kulikua na wasi wasi kutakuwepo na mvutano hadi mwisho wa mkutano hasa baada ya kundi la kumpinga Trump lilipojaribu kuzuia utaratibu wa kanuni kuendelea.

XS
SM
MD
LG