Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 10:32

Sanders amuunga mkono mpinzani wake mkuu Clinton


Wagombea kiti cha rais wa chama cha democratic wa mwaka wa 2016 nchini Marekani, Seneta Bernie Sanders na Hillary Clinton wakiwapungia mkono mashabiki kabla ya kuzungumza pamoja.

Mgombea kiti cha rais wa chama cha Democratic hapa Marekani, Bernie Sanders ametangaza kumuunga mkono mpinzani wake mkuu katika kampeni za kugombania nafasi ya kiti cha rais kwa niaba ya chama hicho.

Sanders akitokea pamoja na Bi Hillary Clinton Jumanne asuhuhi katika mkutano wa kampeni mjini Portsmouth, jimbo la New Hampshire, na kusema kuwa Bi. Clinton anafahamu haja ya kuleta mabadiliko muhimu katika mfumo wa kijamii na kiuchumi hapa nchini.

Sanders amesema Bi Clinton amekubaliana na sehemu kubwa ya ajenda yake ya kutoa huduma bora ya afya kwa Wamarekani kuondoa mfumo wa malipo ya juu katika vyuo vikuu, na kuongeza mshahara wa chini wa ajira hapa nchini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG