Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:18

Waziri Mkuu wa India ziarani Kenya


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, kushoto, na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, right, beat drums at the entrance of State House during an official welcome ceremony for Modi in Dar es Salaam Tanzania, July 10, 2016.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, kushoto, na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, right, beat drums at the entrance of State House during an official welcome ceremony for Modi in Dar es Salaam Tanzania, July 10, 2016.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amesema serikali yake itatafakari kuipatia Tanzania mkopo wa dola milioni 500 kwa ajili ya miradi ya maji alipokua anatia saini mikataba mitano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Miongoni mwa mikataba hiyo ni mkopo wa dola milioni 92 kwa ajili ya mradi wa maji huko Zanzibar. Akizungumza baada ya kutia saini mikataba hiyo, Bw Modi amesema pamoja na Rais John Magufuli wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa ulinzi na usalama hasa katika nyanja ya usafiri wa baharini.

Kiongozi huyo wa India akiwa katika ziara ya baadhi ya nchi za Afrika amesema amekubaliana na Rais Magufuli juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya India na Tanzia katika nyanja nyenginezo ikiwa ni pamoja na kilimo, usalama wa chakula, biashara, gesi ghafi na sekta nyingine muhimu zenye maslahi ya pande zote mbili hasa kuhamasisha ushirikiano wa moja kwa moja kati ya viwanda vya nchin hizo mbili.

Ziara ya Waziri Mkuu wa India, Tanzania
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:16 0:00

XS
SM
MD
LG