Mamlaka ya ushuru nchini Kenya, KRA, ilitangaza siku ya Alhamisi kwamba haikudhamiria kuongeza muda uliowekwa kwa Wakenya kulipa ushuru kupitia mfumo mpya wa komyuta ili kurahisisha ulipaji kodi na ushuru, maarufu kama i-tax. Wakenya wengi walionekana wakipanga foleni ndefu katika afisi za mamlaka hiyo kwenye miji tofauti tofauti nchini humo. BMJ Muriithi alizungumza na mtaalam wa maswala ya ushuru nchini Kenya, Jonnah Andrea, na akamuuliza kuelezea tofauti kati ya mfumo wa ushuru wa zamani, na huo mpya wa i-tax. Sikiliza mahojiano hayo hapa: