Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:18

AU: Masharti ya upinzani yatekelezwa kwa mazungumzo DRC


Maandamano DRC 2
Maandamano DRC 2

Umoja wa Afrika (AU) umetoa mtazamo unaoonyesha umuhimu wa kufanyika kwa mazungumzo kufuatia mgogoro wa kisiasa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Msuhulishi wa AU kwa ajili ya mazungumzo ya kitaifa nchini DRC, Edem Kodjo amesema kwamba baadhi ya masharti yaliowekwa na upinzani kabla ya kushiriki kwenye mazugumzo hayo yamepewa ufumbuzi.

Kodjo amesema kwamba utekelezwaji wa masharti hayo ni pamoja na kuwepo na wajumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye kamati ya upatanishi.

Hata hivyo Kodjo ameelezea kuhuzunishwa kwake na kuchelewa kwa mazungumzo hayo hasa kutokana na kile anachoelezea kuwa ni nia mbaya ya pande zote husika.

Unaweza kusikiliza taarifa ya mwandishi wetu wa DRC Saleh Mwanamilongo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:46 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG